Tuesday, October 8, 2013

Zitto: Mishahara ya Viongozi haipaswi kuwa siri, Waziri Mkuu analipwa takribani Mil 26 bila kodi

Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Mh. Zitto Kabwe (Mb) amesema ni jambo la ajabu serikali kufungia magazeti eti kwasababu limechapisha mishahara ya watumishi wa Serikali. Zitto amesema Kikwete alisaini mkataba wa uwazi wa serikali na Rais Obama miezi michache iliyopita, "sasa kunauwazi gani zaidi ya wananchi kujua mshahara wa Rais wao na Mawaziri" alihoji Zitto. Sasa niwaambie Wananchi wa Mpanda Waziri Mkuu analipwa takribani Milioni 26 na hakatwi kodi, halipi kodi ya nyumba, hanunui nguo yaani ni ajabu. Akifafanua kuhusu mshahara wa Waziri Mkuu Zitto alisema Waziri Mkuu kama Mbunge analipwa Milioni 11.2, Kama Waziri anaongezewa kama Milioni 9.8 na kama Waziri Mkuu anaongezewa tena kama milioni 5 alisema Zitto. Zitto amesema uchochezi unaosemwa na serikali ni tofauti kubwa ya Mishahara na Kodi kwa Watumishi wa Serikali moja wenye majukumu ambayo karibia yanafanana na kiwango cha elimu kinayofanana.

Chanzo:Jamiiforum 

No comments:

Post a Comment