Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Bara, Philip
Mangula, amesema anajuta na anaona aibu kuishi katika Jimbo la Kawe
linaloongozwa na Halima Mdee (Chadema), na kuwataka wanachama wa CCM
kuhakikisha uchaguzi wa mwaka 2015 jimbo hilo linarudi kwao.
Mangula aliyasema hayo jana alipozungumza na viongozi mbalimbali wa kata
na wilaya zote za jijini Dar es Salaam pamoja na viongozi wa mkoa wa
Dar es Salaam wa CCM.
“Ni aibu mimi ni mkazi wa Oysterbay jijini Dar es Salaam, na Mdee ndiye
Mbunge wangu sasa siku akisema anataka kuongea na wazee wa jimbo lake
mimi ntafanyaje? siwezi kwenda nitasingizia naumwa ili nisiende,”
alisema.
Maswali yangu kwake ni haya:
-WanaCCM pekee wa jimbo la Kawe wanatosha kulirudisha jimbo CCM ktk sanduku la kura?
-Kwanini awe mwongo asisngizie kuumwa,kwani hana demokrasia ya kukataa kwenda kwenye kikao?
-Kinachomsababisha ajute ni kipi?
chanzo:Jamiiforum
No comments:
Post a Comment