Mh.Magufuli
anatakiwa kujua kwamba Watanzania wa sasa sio wale wa zamani ambao mtu
angeweza kuwaburuza atakavyo.Sasa hivi Serikali inaendeshwa kwa misingi
ya Utawala Bora.Inashangaza kuona Mh. huyu akitoa majigambo na kumdharau
Waziri aliyekuwa ametoa waraka kuruhusu magari yatumiayo barabara zetu
kupewa msamaha wa uzito unaofikia asilimia tano ya uzito uliowekwa
kisheria.Jambo la kujiuliza ni je,Mh Magufuli kauona lini Waraka
huo?Mbona upo tangu mwaka 2006 na yeye amekuwa Waziri wa Wizara hiyo
tangu lini?Unafiki wa namna hii ni hatari kwa maendeleo ya nchi hasa
pale Serikali inapokuwa na viongozi wa aina ya Mh. Magufuli.Kama
kulikuwa na nia nzuri ya kuchukua hatua ya kuufuta huo Waraka Mh.
Magufuli alishindwa nini kutoa muda kwa wasafirishaji ili wajue kuwa
kuanzia tarehe fulani unafuu uliokuwepo utaondolewa.Viongozi wapenda
sifa na wenye majigambo wanawaumiza wananchi kwa maamuzi yao ya kipuuzi
na yasiyozingatia busara.Kwamba msafirishaji ambaye gari lake tayari
liko njiani atarekebisha vipi mzigo alioubeba kabla ya kufika
mizani?Hapo kuna utawala bora?Sasa hivi tayari wananchi wameanza kupata
adha ya usafiri kutokana na ubabe wa kiongozi asiye na msimamizi!Mtu
huyu anasemekana kuwa anautaka uraisi akiupata nchi hii si itaangamia?
chanzo:Jamiiforum
No comments:
Post a Comment