Thursday, October 10, 2013

Mangula: Najuta kuishi jimbo la Halima Mdee

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Bara, Philip Mangula, amesema anajuta na anaona aibu kuishi katika Jimbo la Kawe linaloongozwa na Halima Mdee (Chadema), na kuwataka wanachama wa CCM kuhakikisha uchaguzi wa mwaka 2015 jimbo hilo linarudi kwao.
Mangula aliyasema hayo jana alipozungumza na viongozi mbalimbali wa kata na wilaya zote za jijini Dar es Salaam pamoja na viongozi wa mkoa wa Dar es Salaam wa CCM.
“Ni aibu mimi ni mkazi wa Oysterbay jijini Dar es Salaam, na Mdee ndiye Mbunge wangu sasa siku akisema anataka kuongea na wazee wa jimbo lake mimi ntafanyaje? siwezi kwenda nitasingizia naumwa ili nisiende,” alisema.

Maswali yangu kwake ni haya:
  -WanaCCM pekee wa jimbo la Kawe wanatosha kulirudisha jimbo CCM ktk sanduku la kura?
-Kwanini awe mwongo asisngizie kuumwa,kwani hana demokrasia ya kukataa kwenda kwenye kikao?
-Kinachomsababisha ajute ni kipi?

chanzo:Jamiiforum

Tuesday, October 8, 2013

Zitto: Mishahara ya Viongozi haipaswi kuwa siri, Waziri Mkuu analipwa takribani Mil 26 bila kodi

Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Mh. Zitto Kabwe (Mb) amesema ni jambo la ajabu serikali kufungia magazeti eti kwasababu limechapisha mishahara ya watumishi wa Serikali. Zitto amesema Kikwete alisaini mkataba wa uwazi wa serikali na Rais Obama miezi michache iliyopita, "sasa kunauwazi gani zaidi ya wananchi kujua mshahara wa Rais wao na Mawaziri" alihoji Zitto. Sasa niwaambie Wananchi wa Mpanda Waziri Mkuu analipwa takribani Milioni 26 na hakatwi kodi, halipi kodi ya nyumba, hanunui nguo yaani ni ajabu. Akifafanua kuhusu mshahara wa Waziri Mkuu Zitto alisema Waziri Mkuu kama Mbunge analipwa Milioni 11.2, Kama Waziri anaongezewa kama Milioni 9.8 na kama Waziri Mkuu anaongezewa tena kama milioni 5 alisema Zitto. Zitto amesema uchochezi unaosemwa na serikali ni tofauti kubwa ya Mishahara na Kodi kwa Watumishi wa Serikali moja wenye majukumu ambayo karibia yanafanana na kiwango cha elimu kinayofanana.

Chanzo:Jamiiforum 

Magufuli,Ubabe katika shughuli za Serikali umepitwa na wakati!

Mh.Magufuli anatakiwa kujua kwamba Watanzania wa sasa sio wale wa zamani ambao mtu angeweza kuwaburuza atakavyo.Sasa hivi Serikali inaendeshwa kwa misingi ya Utawala Bora.Inashangaza kuona Mh. huyu akitoa majigambo na kumdharau Waziri aliyekuwa ametoa waraka kuruhusu magari yatumiayo barabara zetu kupewa msamaha wa uzito unaofikia asilimia tano ya uzito uliowekwa kisheria.Jambo la kujiuliza ni je,Mh Magufuli kauona lini Waraka huo?Mbona upo tangu mwaka 2006 na yeye amekuwa Waziri wa Wizara hiyo tangu lini?Unafiki wa namna hii ni hatari kwa maendeleo ya nchi hasa pale Serikali inapokuwa na viongozi wa aina ya Mh. Magufuli.Kama kulikuwa na nia nzuri ya kuchukua hatua ya kuufuta huo Waraka Mh. Magufuli alishindwa nini kutoa muda kwa wasafirishaji ili wajue kuwa kuanzia tarehe fulani unafuu uliokuwepo utaondolewa.Viongozi wapenda sifa na wenye majigambo wanawaumiza wananchi kwa maamuzi yao ya kipuuzi na yasiyozingatia busara.Kwamba msafirishaji ambaye gari lake tayari liko njiani atarekebisha vipi mzigo alioubeba kabla ya kufika mizani?Hapo kuna utawala bora?Sasa hivi tayari wananchi wameanza kupata adha ya usafiri kutokana na ubabe wa kiongozi asiye na msimamizi!Mtu huyu anasemekana kuwa anautaka uraisi akiupata nchi hii si itaangamia?

chanzo:Jamiiforum