Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Bara, Philip
Mangula, amesema anajuta na anaona aibu kuishi katika Jimbo la Kawe
linaloongozwa na Halima Mdee (Chadema), na kuwataka wanachama wa CCM
kuhakikisha uchaguzi wa mwaka 2015 jimbo hilo linarudi kwao.
Mangula aliyasema hayo jana alipozungumza na viongozi mbalimbali wa kata
na wilaya zote za jijini Dar es Salaam pamoja na viongozi wa mkoa wa
Dar es Salaam wa CCM.
“Ni aibu mimi ni mkazi wa Oysterbay jijini Dar es Salaam, na Mdee ndiye
Mbunge wangu sasa siku akisema anataka kuongea na wazee wa jimbo lake
mimi ntafanyaje? siwezi kwenda nitasingizia naumwa ili nisiende,”
alisema.
Maswali yangu kwake ni haya:
-WanaCCM pekee wa jimbo la Kawe wanatosha kulirudisha jimbo CCM ktk sanduku la kura?
-Kwanini awe mwongo asisngizie kuumwa,kwani hana demokrasia ya kukataa kwenda kwenye kikao?
-Kinachomsababisha ajute ni kipi?
chanzo:Jamiiforum
familia yetu
Thursday, October 10, 2013
Tuesday, October 8, 2013
Zitto: Mishahara ya Viongozi haipaswi kuwa siri, Waziri Mkuu analipwa takribani Mil 26 bila kodi
Naibu
Katibu Mkuu wa CHADEMA Mh. Zitto Kabwe (Mb) amesema ni jambo la ajabu
serikali kufungia magazeti eti kwasababu limechapisha mishahara ya
watumishi wa Serikali. Zitto amesema Kikwete alisaini mkataba wa uwazi
wa serikali na Rais Obama miezi michache iliyopita, "sasa kunauwazi gani
zaidi ya wananchi kujua mshahara wa Rais wao na Mawaziri" alihoji
Zitto. Sasa niwaambie Wananchi wa Mpanda Waziri Mkuu analipwa takribani
Milioni 26 na hakatwi kodi, halipi kodi ya nyumba, hanunui nguo yaani ni
ajabu. Akifafanua kuhusu mshahara wa Waziri Mkuu Zitto alisema Waziri
Mkuu kama Mbunge analipwa Milioni 11.2, Kama Waziri anaongezewa kama
Milioni 9.8 na kama Waziri Mkuu anaongezewa tena kama milioni 5 alisema
Zitto. Zitto amesema uchochezi unaosemwa na serikali ni tofauti kubwa ya
Mishahara na Kodi kwa Watumishi wa Serikali moja wenye majukumu ambayo
karibia yanafanana na kiwango cha elimu kinayofanana.
Chanzo:Jamiiforum
Chanzo:Jamiiforum
Magufuli,Ubabe katika shughuli za Serikali umepitwa na wakati!
Mh.Magufuli
anatakiwa kujua kwamba Watanzania wa sasa sio wale wa zamani ambao mtu
angeweza kuwaburuza atakavyo.Sasa hivi Serikali inaendeshwa kwa misingi
ya Utawala Bora.Inashangaza kuona Mh. huyu akitoa majigambo na kumdharau
Waziri aliyekuwa ametoa waraka kuruhusu magari yatumiayo barabara zetu
kupewa msamaha wa uzito unaofikia asilimia tano ya uzito uliowekwa
kisheria.Jambo la kujiuliza ni je,Mh Magufuli kauona lini Waraka
huo?Mbona upo tangu mwaka 2006 na yeye amekuwa Waziri wa Wizara hiyo
tangu lini?Unafiki wa namna hii ni hatari kwa maendeleo ya nchi hasa
pale Serikali inapokuwa na viongozi wa aina ya Mh. Magufuli.Kama
kulikuwa na nia nzuri ya kuchukua hatua ya kuufuta huo Waraka Mh.
Magufuli alishindwa nini kutoa muda kwa wasafirishaji ili wajue kuwa
kuanzia tarehe fulani unafuu uliokuwepo utaondolewa.Viongozi wapenda
sifa na wenye majigambo wanawaumiza wananchi kwa maamuzi yao ya kipuuzi
na yasiyozingatia busara.Kwamba msafirishaji ambaye gari lake tayari
liko njiani atarekebisha vipi mzigo alioubeba kabla ya kufika
mizani?Hapo kuna utawala bora?Sasa hivi tayari wananchi wameanza kupata
adha ya usafiri kutokana na ubabe wa kiongozi asiye na msimamizi!Mtu
huyu anasemekana kuwa anautaka uraisi akiupata nchi hii si itaangamia?
chanzo:Jamiiforum
chanzo:Jamiiforum
Subscribe to:
Comments (Atom)